Namna gani unaweza kushinda kuwa mpweke bila kupata vishawishi vya ngono?

Kwa watu ambao wanaongea Kiswahili

  1. dontgiveup777

    dontgiveup777 Fapstronaut

    11
    4
    3
    Hili swali nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara na pengine nikipata jibu ya swali hili nitaweza kujua namna gani nzuri ya kuweza kupambana na mawazo kuelekea katika fikra za ngono kila muda. Nimejaribu kuweka notebook ya kuweza kurekodi kila mara ninapoangalia pono, mara nyingi hunitokea wakati wa weekends ambapo ninakuwa sina chochote cha kufanya nyumbani, imefika wakati kwamba naomba hata weekend zisiingie kwa sababu najua kitakachoenda kutokea, huwa nashindwa kujizuia kabisa na mwisho wa siku najikuta nafungua browser, naingia "Private mode" nafungua tabs kadhaa kufanya upekuzi wa video nzuri, muda huu wote nakuwa kama robot, ikishafika hatua nimefungua "private mode" siwezi kuacha mpaka nimalize kila kitu :emoji_wink: , baada ya hapo tu ndio akili inanirudia naanza tena kujilalumu.
    Muda mwingine unakuta ni uchovu tu au stress za siku ambazo zinafanya mawazo yahamie kwenye kuangalia pono na kupulika.
    Haya maisha yamekuwa yakienda kama hivi kwa muda mrefu sasa na sijui ni namna gani ya kuweza kuachana na hii tabia.

    Kwa mtu ambaye anapitia shida kama hii au ameweza kupata namna nzuri ya kupambana na haya mawazo atupie mchango wake, unaweza share experience zako pia katika huu uraibu kwa sababu naona kupambana nao ukiwa peke yako ni kitu kigumu sana